Ndugu wawili raia wa India wanaotuhumiwa kwa ufisadi Afrika Kusini, wakamatwa DubaiNdugu wawili wafanya biashara wazaliwa wa India ambao wanadaiwa kuwa mstari wa mbele kwenye mtandao mkubwa wa ufisadi nchini Afrika Kusini wamekamatwa huko Dubai, serikali ya Afrika kusini imetangaza.


Kukamatwa kwao kunajiri wakati uchunguzi ukikamilishwa kuhusu uporaji mkubwa wa taasisi za serikali wakati wa enzi za rais wa zamani Jacob Zuma.

Wizara ya sheria ya Afrika Kusini “imethibitisha kwamba ilipata taarifa kutoka kwa mamlaka za kisheria katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwamba watoro hao wa sheria, ambao ni Rajesh na Atul Gupta walikamatwa,” wizara hiyo imethibitisha katika taarifa.

Walishtumiwa kutoa hongo na badala yake kupewa kandarasi kubwa za serikali na zenye faida kubwa na kuwa na ushawishi kwenye uteuzi wa mawaziri.

Kukamatwa kwao kunajiri mwaka mmoja baada ya polisi ya kimataifa Interpol kutoa tahadhari ya kuwasaka mwezi Julai mwaka jana.

“Majadiliano kati ya mamlaka mbalimbali za kisheria huko UAE na nchini Afrika Kusini kuhusu kitakachofuata yanaendelea,” imesema wizara ya sheria ya Afrika Kusini.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu