Ndugai aonekana bungeni kwa mara ya kwanzaBaada ya maswali yasiyo na majibu ya aliyekuwa spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Job ndugai alipo na kutokuonekana bungeni,hii leo majibu yamepatikana na kuondoa maswali yote.


Ni baada ya spika huyo mstaafu na mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, kuanza hii leo kuhudhuria vikao vya Bunge la Bajeti 2022/2023 tangu kujiuzulu Uspika January 06 mwaka huu.


Ndugai ameonekana leo ikiwa kinafanyika kikao cha sita cha mkutano wa saba wa Bunge la 12 siku ambayo Bunge linatarajia kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu