Mwanamke aliyevamia taarifa ya habari na bango urusi apotea kusikojulikanaMwanamke anayedaiwa kuwa ni muhariri wa habari wa kituo cha televisheni cha Chanel 01 cha nchini Urusi ameripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha.


Mwanamke huyo Marina Ovsyannikoniva alivamia taaifa a habari ikiendelea katika televisheni hiyo ya Chanel one akiwa na bango linalosomeka "hakuna vita,sitisha vita msiamini propaganda za serikali ya Urusi,wanadanganya hapa".


Kabla ya kuvamia habari inadaiwa mwanamke huyo alijirekodi video akisema "ninajisikia aibu kujiruhusu mwenyewe kusema uongo kupitia televisheni hii,ninajisikia aibu kuruhusu raia wa Urusi kugeuzwa mazombi"


Kuna taarifa zinasema kuwa kwa sasa mwanamke huyo yuko chini a ulinzi wa polisi akisubiri mashtaka ya uchochezi dhidi ya serikali yake Urusi.


Taifa la Urusi limeendelea kutunga na kupitisha haraka sheria ambazo zinawataka raia na vyombo vya habari kuripoti na kuunga mkono kile tu ambacho serikali imekiagiza au kukiamua

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu