Mwanamke aliyefunga ndoa na waume wawili asaka mume wa tatu.Dunia inaendelea kuonesha maajabu yake na hii ni baada ya mwanamke mmoja kuendelea kuitikisa mitandao kwa muda mrefu baada ya uamuzi wake wa kuishi na wanaume wawili kama waume zake wa ndoa.


Mwanamke huyo raia wa Marekani anayefahamika kwa jina la Kenya Stevens (42) anadai kuwa mume wa kwanza Carl Stevens wameishi naye kwa miaka 26 huku mume wa pili anayefahamika kwa jina la Tiger wameishi naye kwa miaka tisa hadi hivi sasa.
Mwanamke huyo pia amewaambia waandishi wa habari kuwa pamoja na kuwa na waume wawili bado anaendelea na uhusiano na wanaume wengine kwa lengo la kutaka kuongeza idadi ya waume ambao ataishi nao kama waume zake.


“ndoa za mke mmoja aliyeolewa na wanaume zaidi ya mmoja inaweza kuwa ngumu katika jamii yatu kwakuwa iliyozoeleka ni ya mke mmoja kuwa na mume mmoja” alisema

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu