Mwanafunzi wa chuo amuua mwenzake kwa wivu wa mapenzi DodomaMwanafunzi wa kike Winfrida Michael (24) aliyekuwa akisoma Chuo cha St John mkoani Dodoma amefariki baada ya kuchomwa kisu na mpenzi wake Julias Gervas (26) ambaye pia ni mwanafunzi wa chuo hicho sababu ikitajwa kuwa wivu wa mapenzi.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno mnamo Septemba 8, 2022 amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kubainisha kuwa bada ya Julius kufanya mauaji hayo alijaribu kujiua kwa kujikata tumbo na sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa Mkoa wa Dodoma.


Ofisa muuguzi wa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Ester Ngoloki amesema Septemba 7, 2022 walimpokea Julias akiwa na jeraha la kuchomwa na kitu chenye ncha kali tumboni.Amesema walimpokea Ester akiwa amefariki na mwili wake ukiwa na majeraha ya kitu chenye ncha kali.


“Majeruhi yupo hospitali akiendelea kupatiwa matibabu na anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji na mwili wa Winjfrida umechukuliwa na ndugu kwa ajili ya taratibu za familia,” amesema.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu