Mwanafunzi ajiua kwa bastola moshi ataka mwili wake uchomwe na uzikwe MarekaniRobert Meier (17) ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari St Mary Goreti iliyopo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, amejiua kwa kujipiga risasi huku akiacha ujumbe akitaka mwili wake uchomwe.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema lilitokea usiku wa kuamkia juzi.


Akisimulia tukio hilo, Kamanda huyo alidai kuwa kabla ya mwanafunzi huyo kujiua, aliacha ujumbe wa maandishi ulisomeka mwili wake uchomwe na majivu yake yasafirishwe kwenda Marekani yakazikwe pembezoni mwa kaburi la baba yake.


Kwa mujibu wa Kamanda Maigwa, baba yake Robert alifariki dunia akiwa Marekani na mwili wake ulizikwa nchini humo.


Kamanda Maigwa alifafanua kuwa siku ya tukio saa 8 usiku wa kuamkia juzi huko Mwereni katika Kata ya Ngangamfumuni, mwanafunzi huyo alijiua kwa kujipiga risasi kifuani upande wa kushoto kwenye moyo na risasi hiyo ikatokea mgongoni.


Alisema alijiua kwa kwa kutumia bastola namba LXE 023 aina ya Glock iliyotengenezwa nchini Austria, inayomilikiwa kihalali na mtu aitwaye Boniface Kimario, mkazi wa Mwereni ambaye Jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahojiano zaidi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu