Mvua kubwa yaua watu 39 AfghanistanUmoja wa Mataifa unasema mvua kubwa na mafuriko yamesababisha vifo vya watu 39 wakiwemo watoto 9 nchini Afghanistan.


Afisi ya Umoja wa Mataifa ya Ushirikishi wa Masuala ya Kiutu OCHA inasema watu wengine 14 wamejeruhiwa. Mvua hizo zimesababisha maporomoko ya ardhi na kufichua mabomu ambayo hayajalipuka yaliyokuwa yametegwa kutokana na miongo minne ya vita na machafuko nchini humo.


Umoja wa Mataifa unasema mabomu hayo yanaondolewa taratibu na kuteguliwa ili kuzuia majeruhi.


Hii ni mara ya tatu eneo la mashariki mwa nchi hiyo limekumbwa na mafuriko chini ya mwezi mmoja. Watu 19 wameuwawa na 131 kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili mnamo mwezi Juni.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu