Mume ajiua baada ya kukutwa akimtongoza mwanamke mwingineKijana John Mhagama (42) mkazi wa mtaa wa kanisa B, wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe amejiua kwa kunywa sumu baada ya kufumaniwa na mke wake akiwa kwenye mazungumzo ya kimapenzi na binti wa kidato cha kwanza anayeishi nyumba jirani na yao.


Imeelezwa kuwa marehemu alikuwa na tabia ya kwenda kununua mkaa kwa jirani kila ifikapo jioni, kumbe alipokuwa akienda huko anakutana na binti huyo na kumpa pesa.


Akizungumzia tukio hilo jana Jumatatu, Septemba 12, 2022, Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo alipozungumza na waandishi wa habari.


“Siku ya tukio marehemu alikwenda kununua mkaa kama kawaida yake, lakini siku hiyo mkewe alikuwa akimfuatulia kwa nyuma na kumuona akiongea na binti na kumpa Sh5,000 huku akimbembeleza kumkubalia ombi lake la mapenzi, kwani amekuwa akichukua pesa zake pasipo kumtimizia,” amesema.


Alisema baada ya mkewe kuwaona alijitokeza na kuanza kumlaumu mumewe kwa kitendo alichofanya, lakini kwa hasira mumewe huyo alimpiga mkewe na kisha kwenda kusokojulikana.


Aliendelea kusema kuwa, baada ya mkewe kuhojiwa na Polisi, alisema mumewe hakurejea nyumbani na ndipo baadaye alipigiwa simu na shangazi wa marehemu akimjulisha kuwa mumewe huyo ana hali mbaya, hivyo alipokwenda kumpeleka hospitali ambako alipoteza maisha.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu