Mtoto wa mwaka mmoja atupwa,akutwa amefarikiMtoto Mchanga wa siku moja amekutwa amefariki katika Mtaa wa amani, Kinyanambo Kata ya Upendo Halmashauri ya Mji Mafinga baada ya wanamke mmoja asiyefahamika kujifungua kisha kumtupa.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa Mtendaji wa Mtaa huo, Majolino Myinga amesema kuwa alipigiwa simu na wananchi wa mtaani hapo baada ya kuona mtoto mwenye jinsia ya kike akiwa amekufa baada ya kutupwa na mtu asiyejulikana katika mtaa huo.


"Tumejaribu kuangalia mtoto huyo tumekuta ameshakufa lakini aliyetupa bado hajulikani tumepeleka taarifa polisi kwa ajili ya kufanya uchunguzi ili waweze kubaini aliyefanya ufanyama huo." Amesema Myinga


Aidha Afisa huyo amesema kuwa matukio hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara katika mtaa huyo ambapo hadi sasa tukio hilo ni la nne la watu wasiyojulikana kutupa watoto katika mtaa hapo.


"Wito wangu kwa jamii kuacha tabia hizi za kinyama ambazo hazikubaliki ndani ya jamii kama mtu anaona mwanaume ambaye amempatia ujauzito huo lakini anashindwa kumsaidia ni bora atoe taarifa katika ofisi za Serikali kwa sababu hali hii haitupendezi hata kidogo." Amesema Afisa huyo


Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo, Mernkon Ndelwa amesema tangu mwaka jana matukio hayo yameanza kujitokeza akina mama kutupa watoto wachanga lakini hadi sasa bado hawafahamiki wanatoka katika maeneo gani.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu