Msaidizi wa kazi akamatwa kwa mganga wa kienyeji ili asikamatwe kwa wiziDada msaidizi wa kazi za nyumbani anayedaiwa kuiba Sh milioni 4 kwa muajiri wake nchini Kenya amekamatwa akiwa kwa mganga wa kienyeji akifanyiwa dawa ili asikamatwe.


Dada huyo ambaye polisi nchini humo hawakumtaja jina wanasema walimkuta akiwa juu ya kaburi kwenye karai akiwa amememwagiwa damu ya ndege akiwa amefumba macho wakati mganga akiendelea na tiba hiyo.


Inadaiwa mganga ili kuwazubaisha polisi aliendelea kufanya hicho kinachoitwa tiba kwa mteja wake huyo kwa kuongea maneno yasiyoeleweka mfululizo bila kuacha hadi hapo askari walipokata shauri na kumkamata.


Anadaiwa aliiba pesa hizo kutoka kwa muajiri wake katibu kkuu wa utawala wa hazina Nelson Gaichuhie .


Amekamatwa siku ya Jumatatu kwa mganga huko Gachie, ambapo alikuwa ameenda kutafuta ulinzi pamoja na mumewe.


Kufuatia kukamatwa, maafisa wa upelelezi walipata Sh1.57 milioni katika nyumba ya mamake katika kaunti ya Murang'a.


Mbali na fedha pia askari walifanikiwa kupata vito vya thamani vilivyokuwa vimeibiwa.


Mnamo mwezi Juni, CAS Gaichuhie na mkewe Charity Waithera waliwaambia polisi kuwa waliacha Sh6 milioni kwenye kabati lao la nguo lakini waligundua Sh4 milioni zikiwa hazipo waliporejea nyumbani.


Vito vya thamani ya Sh500,000 pia havikuwepo na msaada wa nyumba.


Wanandoa hao waliripoti wizi huo kwa kituo cha polisi cha Hardy na polisi wakaongozana nao hadi nyumbani kwao ambapo polisi walibaini kuwa hakukuwa na uvunjaji.Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu