Msalaba mwekundu wafanikiwa kuziunganisha familia 300 za wanajeshi UkraineShirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limesema limefanikiwa kuwasiliana na familia 300 ndani ya Urusi na Ukraine juu ya jaala za ndugu zao wanaoshikiliwa mateka.


Mkurugenzi wa shirika hilo, Robert Mardini, amewaambia waandishi wa habari kwamba kazi ya kuwafuatilia watu waliopotea inaendelea vyema.


Hata hivyo, hakutowa undani kuhusiana na jaala ya Warusi na Waukraini hao 300, lakini alisema familia zao zilikuwa na masuali muhimu waliyotaka majibu juu ya ndugu zao hao.


Mkurugenzi huyo alisema pia kuwa kumepatikana mafanikio kwenye haki ya shirika lake kuwatembelea wafungwa wa kivita, ambayo ni sehemu ya mkataba wa Geneva. Shirika la Msalaba Mwekundu liliwasajili wanajeshi wote wa Ukraine waliojisalimisha kwa Urusi kutoka katika eneo la viwanda la Azovstal mjini Mariupol.


Urusi inasema jumla ya wapiganaji hao walikuwa 2,439.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu