Mkuu wa Ujasusi Ufaransa kufukuzwa kisa kushindwa kutambua mapema uvamizi wa Urusi UkraineMkurugenzi wa ujasusi wa kijeshi wa Ufaransa, Jenerali Éric Vidaud, yupo katika hatari ya kufukuzwa kazi kwa tuhuma za kupuuza taarifa za uwezekano wa Urusi kuivamia Ukraine.

Kikinukuu chanzo cha ndani cha Wizara ya Majeshi, chombo cha habari cha l'Opinion kimesema Jenerali Vidaud atafukuzwa kazi kwa sababu ya "maelezo yasiokidhi mahitaji" na "ukosefu wa uelewa".


Mkuu wa Majeshi ya Ufaransa, Thierry Burkhard, alikiri katika mahojiano na Le Monde kwamba hatua hiyo inakuja wakati idara za kijasusi za Ufaransa - ikiwa ni pamoja na Vidaud - ziligundua kuwa zilifanya uchambuzi wa kimakosa wa tishio la Urusi nchini Ukraine, ambalo lilienda kinyume na tathmini ya Amerika.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu