Mke ajinyonga kwa kitenge baada ya kumshabulia mumewe kwa pangaMkazi wa kitongoji Kijiji cha Sibwesa wilayani Tanganyika, Mande Emanuel (30) amejinyonga baada ya kumjeruhi mumewe, Dotto Enos (35) kwa kumkata mapanga.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumapili Machi 20, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kifamilia uliosababishwa na shughuli za kilimo.


“Ilitokea sintofahamu ikapelekea ugomvi kutokea ndipo mwanamke huyo aliamua kumpiga mapanga mume wake na kumjeruhi vibaya,”


“Alipogundua mume wake anaweza kufa akahofia kupata kesi ya mauaji, alizunguka nyuma ya nyumba yao akapasua kitenge chake akajinyonga, mume alipelekewa hosptali ya rufaa mkoa kutibiwa,” amesema Kamanda Makame

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu