Mfungwa aliyebadili jinsia awapa ujauzito wafungwa wenzake wawili,ahamishwa gereza.Mfungwa aliyebadili jinsia ambaye aliwapa wafungwa wenzake wawili mimba katika gereza la pekee la wanawake la New Jersey amehamishwa na kupelekwa katika gereza la wanaume.


Demi Minor, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 30 kwa kumchoma kisu baba yake na kumsababshia kifo, alihamishwa kutoka gereza la wanawake la Edna Mahan hadi gereza la Garden State mwezi Juni.


Minor, 27, analalamika kwamba alidhulumiwa haki na askari wakati akihamishwa na hata aliwekwa katika uangalizi maalumu baada ya kufanya jaribio la kujitoa uhai kwa kujinyonga alipokuwa akihamishiwa katika gereza la wanaume.


Katika chapisho kwenye blogu yake ya Justice 4 Demi, Minor alidai kwamba aliandamwa na maafisa wa kurekebisha tabia, huku mmoja wao akimdhihaki alipoomba kuvuliwa nguo na kupekuliwa na mwanamke.


Katika chapisho tofauti, alidai alipigwa wakati wa uhamisho.


Alisema alizuiliwa kwa muda katika Gereza la Jimbo la New Jersey, ambapo walinzi walidaiwa kumuita 'a he' zaidi ya mara 30.


Kesi ya Minor ilipata sifa mbaya mnamo Aprili wakati Idara ya magereza ya New Jersey ilipofichua kwamba alikuwa amewapa mimba wafungwa wenzake wawili katika Kituo cha Kurekebisha Tabia cha Edna Mahan.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu