Mchungaji wa kike aliyemuoa mwanamke mwenzake azuiwa kuongoza ibada kwa hiliMchungaji wa kike Mpho Tutu van Furth ambaye ni Binti wa Marehemu Askofu Desmond Tutu, jana alizuiliwa na Kanisa la England kuongoza mazishi sababu ameoa mwanamke mwenzie.


Mpho alifunga ndoa na Marceline Desemba 2015 na alilazimishwa kuacha kufanya kazi kama Mchungaji nchini Afrika Kusini.


Mwanamama huyo ni Mchungaji wa Dhehebu la Anglikana katika Dayosisi ya Washington na alikuwa akijiandaa kuongoza mazishi ya Marehemu baba yake wa kiroho.Binti Tutu aliliambia Shirika la habari la BBC kuwa "hali hii ni mbaya na inaumiza", huku dayosisi ikisema hii ni hali ngumu.


Kanisa la England haliruhusu wachungaji wake kuwa kwenye ndoa za jinsia moja sababu mafundisho yake rasmi ni kuwa ndoa ni kati ya mwanaume mmoja na mwanamke mmoja. Hata hivyo Kanisa la Anglikana la Marekani linaruhusu suala hilo.


Baba yake Desmond Tutu, aliyefariki Desemba 2021, alishinda tuzo ya amani ya Nobel mwaka 1984 kwa mapambano yake dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Pia alifanya kampeni kuunga mkono haki za wapenzi wa jinsia moja na kuunga mkono ndoa zao.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu