Mbunge akemea wanaume wanaonyonya maziwa ya wake zaoMbunge wa Viti Maalum (CCM), Jacqueline Msongozi amesema kitendo cha wanaume kunyonya maziwa ya wake zao ni kuwatesa watoto wao.


Mbunge huyo ameyasema hayo Jumatatu Mei 30, 2022 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa mwaka 2022/2023.


Jacqueline amesema kuwa wanaume hao wanaonyonya maziwa ya wake zao, wanadhulumu haki ya watoto ya kupata virutubisho vinavyotokana na maziwa hayo.


“Na hii imejitokeza katika mikoa mbalimbali. Niombe wizara ifanye utafiti. Yako majibaba yanafakamia maziwa ya watoto. Wanawanyonya maziwa ya wake zao wanaonyonyesha badala ya mtoto kunyonya ili kupata ile lishe,”amesema.


Amesema wananyonya kwasababu maziwa hayo yanavirutubisho vingi na pia inasaidia kukata kilevi (hangover) kwa wanaume wanaokunywa pombe.


“Niombe wizara iweke mpango mzuri na itoe elimu vizuri ili wakinababa hawa wasiwadhulumu watoto hawa haki yao,”amesema.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu