Mbunge akamatwa kwa kumpiga risasi dereva wa mpinzaniMbunge maarufu magharibi mwa Kenya Didmus Barasa amekamatwa kwa madai ya kumpiga risasi dereva wa mpinzani wake wakati wa zoezi la kuhesabu kura.


Barasa na mpinzani wake walikuwa wakifuatilia hesabu ya kura na mzozo ukazuka uliopelekea mpinzani wake kuondoka kwenye ukumbi.


Kamanda wa polisi katika kaunti ya Bungoma Joseph Ondoro amesema kwamba “Barasa alimfuata mpinzani wake aliyekuwa anaingia kwenye gari lake na kumuamuru aondoke kwenye kituo hicho lakini dereva wa mpinzani alikataa kuwasha gari na hapo ndipo Barasa akachomoa bastola na kumpiga risasi dereva.”

Madaktari walithibitisha kwamba amefariki alipowasili kwenye hospitali ya Kimilili.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu