Mbivu mbichi urais Kenya,Odinga ,Ruto watajwa kuchuana vikaliWapiga kura nchini Kenya leo wanashiriki uchaguzi mkuu wa rais na viongozi wengine. Kiti cha urais kinawaniwa na wagombea wanne ambao ni mwanasiasa mkongwe Raila Odinga, Makamu Rais William Ruto, George Wajackoyah na David Mwaure.


Kura za maoni za awali kabla ya uchaguzi zimetabiri ushindani utakuwa mkali kati ya Odinga na Ruto.


Jumla ya wapiga kura milioni 22 wamejiandikisha kushiriki uchaguzi wa leo utakaohitimisha utawala wa rais Uhuru Kenyatta.


Katika kura ya leo, tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC ilitangaza kuahirisha uchaguzi wa magavana wa Mombasa na Kakamega, kwa madai ya hitilafu katika karatasi za kupigia kura.


Uchaguzi mwingine uliofutwa ni ule wa viti vya ubunge vya Kacheliba na Pokot Kusini.


Suala la kupanda kwa gharama za maisha, ufisadi uliokithiri ni miongoni mwa masuala yatakawasukuma wapiga kura.


Matokeo rasmi ya uchaguzi huo yatatangazwa ndani ya wiki moja baada ya uchaguzi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu