Mazishi ya kitaifa ya malkia Elizabeth kufanyika leo LondonBaada ya siku kadhaa za kuaga, mwili wa marehemu Malkia Elizabeth II utaanza safari yake ya mwisho baada ya saa chache kama sehemu ya mazishi makubwa ya serikali.


Mwili utasafirishwa kwanza hadi Westminster Abbey kwa ibada ya kidini mbele ya maelfu ya watu, na kisha kuelekea kasri la Windsor kwa ibada ya ki familia na watu wa karibu zaidi, hatimaye, maziko ya kibinafsi.


Itakuwa siku ya hisia mbalimbali ikiwemo huzuni kubwa, Hali ambayo haijashuhudiwa tangu mazishi ya mwisho ya kitaifa, yale ya Winston Churchill, karibu miaka 60 iliyopita.


Umbali mfupi, kutoka Westminster Abbey, milango itafunguliwa kwa wageni kuanza kuwasili kabla ya ibada ya kidini mapema leo.


Wakuu wa nchi kutoka kote ulimwenguni wamekuwa wakiwasili kuungana na washiriki wa familia ya Kifalme kukumbuka maisha na huduma ya Malkia.


Wanasiasa wakuu wa Uingereza na mawaziri wakuu wa zamani pia watakuwepo.


Wanachama wa familia za kifalme kutoka kote Ulaya, ambao wengi wao walikuwa ndugu wa damu wa Malkia wanatarajiwa - Mfalme Philippe wa Ubelgiji na Malkia Mathilde na Mfalme Felipe wa Uhispania na Malkia Letizia watakuwa huko.Pia viongozi mbalimbali kutoka Afrika tayari wamewasili.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu