Marekani yatekeleza shambulizi la bomu nchini SomaliaJeshi la Marekani limewaua wapiganaji 2 wa Al Shabaab baada ya shambulio la anga kusini mwa Somalia, kulingana na Kamandi ya Marekani ya Afrika.


Majeshi ya Marekani yalikuwa yakisaidia wakati wa operesheni ya majeshi ya Somalia.


Shambulio hili limetokea katika kijiji cha Labikus eneo la Juba ya Chini nchini Somalia, na ni shambulio la pili ambalo Marekani imetekeleza nchini Somalia tangu Rais Joe Biden atangaze kuwa mamia ya wanajeshi wake wanaondoka Somalia.


Kamandi ya Marekani ya Afrika (Africom) ilisema kuwa shambulio hilo la bomu lilitekelezwa wakati Al-Shabaab iliposhambulia vikosi vya Somalia.


Uharibifu uliosababishwa na shambulio hilo haujajulikana, lakini Africom ilisema kuwa hakuna raia aliyejeruhiwa na shambulio hilo.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu