Marekani yatangaza homa ya nyani kama gonjwa la dharuraMarekani imetangaza mlipuko unaoendelea wa Homa ya Nyani kuwa dharura ya afya ya umma, haya ni kwa mujibu wa Maafisa wa nchi hiyo.


Mkuu wa idara ya afya na huduma za kibinadamu nchini Marekani, amesema Taifa hilo sasa litaimarisha hatua zake dhidi ya ugonjwa huo na kuwahimiza raia nchini humo kutopuuza virusi hivyo.


Hatua hizo zitawezesha ufadhili zaidi wa Serikali na kutoa muongozo katika kupambana na ugonjwa huo, tangazo hilo linakuja baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kutoa tangazo sawa na hilo.


Mlipuko wa ugonjwa huo tayari umesababisha maambukizi ya zaidi ya Watu elfu 6 nchini Marekani ambapo Wabunge Democratic wamemshtumu Rais Joe Biden kwa kutochukuwa hatua za haraka kuthibiti mlipuko huo.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu