Mapigano ya magenge hasimu ya uhalifu yakimbiza raia Haiti, 20 wauawaRaia wa haiti katika Mji Mkuu wa nchi hiyo Port-Au-Prince hapo wameyakimbia makaazi yao baada ya makabiliano ya risasi kuibuka kati ya makundi hasimu ya uhalifu.


Haya ni kwa mujibu wa mashuhuda wa shirika la habari la Reuters.


Milio ya risasi ilisikika katika mtaa wa mabanda wa Cite Soleil ambapo watu walionekana kuacha makaazi yao na kukimbia.


Baadhi walioenakana wakikimbia na kuinua mikono yao ili wasishambuliwe.
Makabiliano kati ya makundi ya wahalifu yaliyojihami wiki iliyopita yalipelekea vifo vya karibu watu 20.


Mamlaka ya ulinzi wa raia ya Haiti imesema mapambano hayo yalikuwa kati ya kundi linalojiita Chen Mechan na jengine kwa jina 400 Mawozo ambalo lilihusika katika utekaji nyara wa wamishonari wa Kimarekani na Canada mnamo mwezi Oktoba.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu