Manusura tetemeko la Ardhi wakosa chakulaWatu wengi walionusurika na tetemeko baya zaidi la ardhi nchini Afghanistan katika zaidi ya miongo miwili leo walikuwa hawana chakula, malazi na maji huku wakisubiri katika vijiji vilivyoharibiwa kwa wafanyakazi wa msaada kuwafikia na mvua kubwa ikizidisha masaibu yao.


Tetemeko la ardhi lililokuwa na ukubwa wa 5.9 katika kipimo cha Ritcha mnamo Jumatano, lilipiga zaidi katika eneo lenye milima la mashariki katika mpaka na Pakistan na kuwaua zaidi ya watu 1,000 na kuwaacha maelfu ya wengine bila makazi.


Vijiji vyote vimesambaratishwa katika baadhi ya wilaya zilizoathirika zaidi, ambapo walionusurika wanasema walikuwa wakihangaika hata kutafuta vifaa vya kuwazika wafu wao.


Maafisa wanasema karibu nyumba 10,000 ziliharibiwa, hii ikiwa ni idadi ya kutisha katika eneo ambalo wastani wa watu katika nyumba moja ni zaidi ya 20.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu