Mama adaiwa kumuua mwanaye kwa kumchapa fimboMkazi wa Kibosho Kirima Juu, Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro anadaiwa kumuua mtoto wake mwenye umri wa miaka mitatu na miezi sita, kwa kumchapa kwa fimbo, akimtuhumu kuchezea maji.


Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 27, anadaiwa kufanya mauaji hayo jana Jumapili, Julai 31, 2022, ambapo alimchapa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake.


Inadaiwa alimchapa mtoto huyo akimtuhumu kuchezea maji ya baridi, yaliyokuwa yakitiririka kwenye bomba.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (RPC), Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


Amesema jina la mwanamke huyo ambaye tayari amekamatwa limehifadhiwa.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu