Mali kusitisha ubadilishaji wanajeshi wa kulinda amaniSerikali ya Mali imesema itasitisha ubadilishaji wa wanajeshi wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MINUSMA.


Wizara ya Mambo ya Nje ya Mali imesema uamuzi huo pia unahusisha ubadilishanaji ambao tayari umepangwa. Tangazo hilo la jana limekuja siku nne baada ya serikali nchini Mali kuwakamata wanajeshi 49 wa Ivory Coast, ikiwataja kuwa mamluki, lakini Ivory Coast ilisema walikuwa sehemu ya mzingo wa tano wa MINUSMA.


Msemaji wa MINUSMA Olivier Salgado, alithibitisha kuwa wanajeshi hao walikuwa wanafanyia kazi kampuni ya Ujerumani iliyopewa kandarasi na ujumbe huo.


Umoja wa Mataifa umejibu tangazo la Mali kwa kutoa wito wa kutatuliwa haraka mzozo huo.


Utawala wa kijeshi uliotwaa madaraka nchini Mali Agosti 2020, umewekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya, kutokana na kuchelewesha uchaguzi. Pia umelaumiwa kwa ushirikiano wake wa kiusalama na mamluki wa Urusi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu