MAKALA: Majuto ya wanajeshi waliomnyonga Saddam Hussein ,wanaamin walimsaliti baba asiye na hatiaHuzuni,majonzi na mioyo yao kujisikia ni yenye hatia ya usaliti kwa rafiki wa karibu na mshauri, viliwaandama wanajeshi kumi na mbili wa marekani waliokuwa wameteuliwa kumlinda rais Saddam Hussein Abd Al-Majid Al-Tikrit ama Sadam Hussein wa Iraq baada ya tukio la kuuawa kwa kunyongwa kwa rais huyo.


Wanajeshi hao licha ya kutakiwa kutekeleza jukumu lao la ulinzi wa askari kwa mtuhumiwa au mfungwa katika siku zote kabla ya kunyongwa kwa rais huyo walitengeneza urafiki kiasi cha kumuona kama ni kiongozi na babu yao na sio muuaji.


Mwanajeshi mmoja Will Barden Werper anasema saddam alikuwa anamatumaini mpaka siku zake za mwisho kuwa asingenyongwa na alipanga siku moja kuja kufunga ndoa tena na kuanza maisha yake mapya.


Masikini ,haikuwa hivyo hasa pale usiku wa tarehe 30 disemba 2006, Saddam Hussein alipoamshwa majira ya saa tisa usiku kwenda kukabiliwa na kifo chake kwa kunyongwa.Usiku huo baada ya kuamshwa na kuelezwa habari hizo kuwa anakwenda kunyongwa,saddam alioga taratibu na kujiandaa kukabiliana na kifo hicho.


Mwanajeshi huyo will bardenwerper askari mmoja wapo kati ya hao kumi na mbili kupitia kitabu alichokiandika cha (The Prisoner In His Palace) yani 'mfungwa ndani ya kasri lake, anasema wakati alipomkabidhi saddam hussein kwa askari wenzake waliokuwa na jukumu la kumnyonga, wanajeshi wote kumi na mbili waliokuwa wanamlinda walibubujikwa na machozi machoni mwao.


Mwanajeshi huyo Bardenwerper kupitia kitabu chake hicho The Prisoner In His Palace) anamnukuu mmoja wa wanajeshi wenzake, Adam Rogerson, akisema kuwa , 'hatukuwahi kumuona saddam kama muuaji katili . Alionekana kama babu yetu.


Wanajeshi hao kumi na mbili walitambulika kama 'Super Twelve' waliochaguliwa kutoka katika kundi la wanajeshi mia tano hamsini na moja waliokuwa nchini iraq kuhakikisha uongozi wa sadam unaondoka madarakani na sadam mwenyewe kutiwa nguvuni.


Wanajeshi wale walifanikiwa kuuzima utawala wa saddam na pia kumtia nguvuni ambapo alishitakiwa mahakamani kwa kuamuru mauaji ya wapinzani wake 148 ,mashtaka yaliyozaa hukumu ya kifo kwa kunyongwa.


Mmoja wa askari hao, Steve Hutchinson, aliamua kujiuzulu nafasi yake ndani ya jeshi la marekani baada ya saddam kunyongwa, akionekana kutofurahia kitendo cha baadhi ya raia wa iraq waliokuwa wakiudhihaki mwili wa kiongozi saddam.


Inadaiwa baada ya saddam kunyongwa, mwili wake ulitolewa nje, umati uliokuwepo nje walimtemea mate.Askari huyo baada ya kujiuzulu akatajwa kujivunia kitendo cha kutojihusisha na wairaqi hao waliofanya dhihaka hasa kwa mwili huo wa Saddam Hussein.

Dakika chache kabla ya kunyongwa, saddam alimuita mwanajeshi huyo aliyejiuzulu baada ya kifo chke ,Steve Hutchinson aliyekuwa nje ya seli yake na kumpatia saa yake aina ya 'Raymond Weil'.


Hutchinson alipotaka kukataa kuipokea saa ile, saddam alimlazimisha kupokea ambapo akari huyo aliikubali na kuitunza.


Mpaka leo unaambiwa saa hiyo inafanya kazi na ipo nyumbani kwa askari huyo Hutchinson huko Georgia Marekani.


Mwanajeshi mwingine Adam Rogerson, mmoja wa askari hao alimueleza askari mwenake Will Bardenwerper mtunzi wa kitabu hicho kuwa 'baada ya saddam kunyongwa, walijiona ni kama wamemsaliti saddam.


'Tulijiona kama sie ndio wauaji wake. Uilijiona tumemuua mtu ambaye alikuwa karibu yetu'.


Kitabu hicho cha mwanajeshi Will Bardenwerper kinasema katika kipindi ambacho wanajeshi hao walipokuwa na saddam walijitahidi kumfanya kuwa na furaha.


Wanajeshi hao walimuwekea mpaka bendera ndogo ya iraq chumbani kwake ,lengo likiwa ni kuweka mazingira ya gereza na chumba chake yafanane na ofisi ya kiongozi wa serikali.


Inadaiwa siku ya kwanza sadam anaingia katika chumba hicho, askari mmoja alikimbia haraka kwenye meza na kufuta vumbi ambapo saddam alitabasamu na kukaa.


Saddam alipenda sana kuvuta sigara aina ya 'cohiba', ambazo alizitunza katika kijisanduku cha karatasi zenye unyevunyevu za (wet wipes).

alikuwa anasema kuwa miaka iliyopita, Fidel Castro alikuwa amemfundisha kuvuta sigara.Mwanajeshi Bardenwerper ameeleza kuwa Saddam alipenda sana kutengeneza bustani na alikuwa akipenda hata kupalilia na kukitengeneza kichaka kilichokuwa kinaota katika mazingira ya gereza na kukifanya kama maua.


Mbali na hivo pia sadam alipenda kusikiliza nyimbo za mwanamuziki wa nchini marekani Mary J. Blige na alipenda kuendesha baiskeli yake ya mazoezi ya mwili, ambayo alikuwa akiita 'Pony'.


Urafiki na wanajeshi hao uliendelea kukuwa siku hadi siku na kuna siku saam alimpatia zawadi ya suti mwanajeshi mmoja anayefahamika kwa jina la dawson.


Askari huyo dawson kuna siku aliivaa na wenzake wakamcheka kutokana na size kuwa kubwa ikilinganishwa na umbo lake.


Askari Bardenwerper katika kitabu chake hicho anasema, 'kwa siku kadhaa tulimcheka dawson, kwasababu alikuwa anavaa suti ile na kutembea kana kwamba alikuwa anatembea kwenye onyesho la 'mitindo ya mavazi' .'


Mwanajeshi mmoja alimwambia Saddam kuwa kaka yake amefariki na aliposikia taarifa hizo saddam alimkumbatia na , akamwambia 'kuanzia leo unichukulie kama kaka yako.'


Saddam hakuishia hapo akamwambia askari mwingine kwamba iwapo nitaruhusiwa kutumia pesa zangu. Niko tayari kulipa ada ya elimu ya chuo ya mtoto wako wa kiume.Siku moja wakati wanapiga soga askari hao na saddam ,saddam akawapa hadithi ya namna alivyochukizwa na kitendo cha mwanaye aitwaye uday saddam husein .


Uday Hussein alifyatua risasi katika umati wa watu waliokuwa katika sherehe, ambapo watu wengi waliuawa na wengine wengi walijeruhiwa.


Saddam alikasirika sana kutokana na hilo aliagiza magari yote ya kijana wake huyo uday yateketezwe kwa moto.


Saddam mwenyewe alicheka alipokuwa akituambia alivyochoma magari ya gharama kubwa ya uday kama vile rolls-royce, ferrari na porsche na kushuhudia miale ya moto ikitoka kwenye magari hayo.


Ameandika Barden Werper


Sadam aliondolewa madarakani baada ya majeshi ya marekani kauingia katikati ya mji mkuu wa iraq baghdad na kuanza mapigano na waliomuunga mkono saddam mapigano ambayo walishinda na kufanikiwa kumkamata akiwa amejificha katika shimo.


Ilikuwa ni tarehe 16 march 2003 kabla ya kuondoshwa madarakani walikutana rais bush wa marekani, waziri mkuu wa uingereza tony blair na waziri mkuu wa hispania aznar nchini hispania.


Kutokana na shutma za kuwa na silaha hatari za maangamizi,na shutma za udkteta walizomshutumu nazo walimpa saddam hussein muda wa saa 24 aweamejiuzulu ama aende uhamishoni ambapo saddam hakukubali.


Na aprili 9 , 2003 majeshi ya marekani yaliingia katikati ya mji wa baghdad. Na utawala wa miaka 24 wa saddam hussein ukafikia mwisho.Saddam Hussein Abd Al-Majid Al-Tikrit alizaliwa 28 appril 1937 huko al awja,tikrit nchini iraq na kufariki dunia kwa kunyongwa december 30, 2006 na kuzikwa taehe 31 dec 2006 Tikrit.

Alihufumunkama rais huko nchini iraq akiwa ni raisi wa tano tangu 16 july 1979 hadi 9 april 2003.


Kaka wa saddam na baba yake walifariki kabla ya saddam kuzaliwa,yani mama wa saddam aikuwa mjamzito ujauzito huo ndio huyo saddam.


Baba na kaka wa saddam walifariki kwa ugonjwa kansa.


Hali hiyo ilimsukuma mama wa saddam Bi Subha Tulfah Al-Mussallat kufanya jaribio la kuutoa ujauzito na kujiua kutokana na kupotea wale waliokuwa muhimu kwake.


Baada ya kushindwa kwa jaribio hilo na kujifungua mtoto ambaye ndiye saddam, mjomba wa saddam huku mama yake akiolewa tena mna mwanaume mwingine.Kuna mengi ya kusimulia kuhusu kiongozi huyo,ila kwa sasa tunaihia hapa.Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu