Majeshi ya Urusi yatuhmiwa kubaka wasichana wadogo wa UkraineBalozi wa Ukraine nchini Canada ameyatuhumu majeshi ya Urusi kwa ubakaji wa wasichana wadogo katika taifa la Ukraine.


Balozi huyo Yulia Kovaliv amesema ni sharti Urusi iwajibishwe kwa vitendo hivyo vya uhalifu wa kingono dhidi ya watoto nchini Ukraine.


Yulia Kovaliv ameiambia kamati ya bunge la Canada kwamba Urusi inatumia uhalifu wa kingono kama silaha ya vita na kudai ubakaji ni sharti uchunguzwe kama uhalifu wa kivita.


Kovaliv vile vile amesema majeshi hayo ya Urusi pia yamewateka nyara watoto wa Ukraine na kuwapeleka katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Urusi na hata nchini Urusi kwenyewe.


Kulingana na balozi huyo, Ukraine inashirikiana na washirika ili kuwarudisha watoto hao nchini mwao.


Haya yanafanyika wakati ambapo spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi akiwa amerudi nchini humo kutoka ziara ya ghafla ya mjini Kyiv.


Pelosi anasema bunge la Marekani linahitajika kufanya kazi ya ziada ili kuisaidia Ukraine kupambana na Urusi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu