Maiti zaripotiwa kutapakaa kila kona Ukraine (Mauripol)Mbunge wa Ukraine kutoka jiji la Mariupol Yaroslav Zhelezniak amesema maiti za binadamu zimetapakaa katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo ikiwemo barabarani huku baadhi yake ikizikwa kwenye makaburi ya pamoja.


Picha zinaonyesha jiji hilo likiwa magofu matupu, huku vitongoji vikiwa vimeharibiwa vibaya .


Meya wa jiji hilo Vadym Boychenko, ameesema zaidi ya 80% ya majengo ya makazi yameharibiwa na baadhi yake hayawezi kukarabatika .


Takriban wakaazi 300,000 wamekwama ndani, bila umeme, maji ya bomba ,chakula na vifaa vya matibabu vikipungua.


Uvamizi huo unaelezwa kuwa unaweza kuwa mbaya zaidi, na watu kuwa na njaa na magonjwa kuenea.


Mariupol imezungukwa na majeshi ya Urusi, ambayo yamezuia uundaji wa korido za kuruhusu usambazaji wa misaada ya kibinadamu.


Mariupol imezungukwa na majeshi ya Urusi, ambayo yamezuia barabara za usambazaji wa misaada ya kibinadamu.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu