Mahakama yaamuru kina Mdee waendelee na ubunge hadi itakapokamilisha maamuzi.Mahakama kuu Kanda ya Dar es salam imesema wabunge 19 waliovuliwa uanachama na chama cha demorasia na maendeleo (Chadema ) waendelee na ubunge wao hadi mahakama hiyo itakaposikiliza maombi yao ya zuio la kuvuliwa ubunge.


Jaji John Mgeta ametoa uamuzi huo na kusema shauri hilo litatajwa tena 13 June 2022.


Maombi hayo ya zuio la muda la ubunge wao, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), yamesikilizwa leo Jumatatu, Mei 16, 2022 na Jaji John Mgetta, kuanzia saa 8 mchana.


Wanachama hao wa zamani wa Chadema, Halima Mdee na wenzake 18 walivuliwa rasmi uanachama wa chama hicho, usiku wa kuamkia Mei 12, 2020, baada ya Baraza Kuu la Chadema kutupilia mbali rufaa zao walizozikata wakipinga uamuzi wa Kati Kuu iliyowavua uanachama.


Baraza Kuu la Chadema, ambalo ndilo chombo cha juu kabisa cha maamuzi ya Chadema lenye uamuzi wa mwisho katika kikao chake hicho liliunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu.


Kamati Kuu ya Chadema iliwavua uanachana Novemba 27, 2020, iliyowatia hatiani kwa kosa la kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama.


Hata hivyo, hawakukubaliana na uamuzi huo, badala yake wamefungua maombi ya kibali cha kufungua kesi kupinga uamuzi huo wa Baraza Kuu kutupilia mali rufaa zao na kubariki uamuzi wa Kamati Kuu, kuwavua uanachama.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu