Mahakama ya DRC yabatilisha kifungo cha msaidizi wa raisMahakama ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebatilisha kifungo cha miaka 13 jela kwa aliyekuwa mkuu wa wafanyakazi wa Rais Felix Tshisekedi, Vital Kamerhe, ambaye alipatikana na hatia ya matumizi mabaya ya fedha.


Mahakama ya Cassation ilisema hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa ya Kinshasa/Gombe "ilitiwa dosari za kiutaratibu".

''Mahakama ya Uchunguzi iligundua kuwa Mahakama ya Rufaa ya Kinshasa/Gombe ilikiuka Kifungu cha 104 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kwa kuchunguza kesi hiyo wakati haikuwa sawa,” ilisema Radio Okapi.


Kamerhe alikuwa amepinga muundo wa mahakama na tayari alikuwa amewasilisha kesi hiyo kwa Mahakama ya Kikatiba, kwa mujibu wa tovuti.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu