Mafuriko yaua takribani watu 60 Afrika kusinWatu takribani 60 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyosababishwa na mvua kubwa katika mji wa Durban na maeneo ya jirani ya mkoa wa Kwazulu Natal nchini Afrika Kusini.


Taarifa ya mamlaka ya mji wa Durban imesema mafuriko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa makaazi na miundombinu kutoka maeneo ya vijijini, vitongoji hadi maeneo ya kifahari.


Mvua zilizonyesha kwa siku kadhaa zimesababisha maeneo kufurika, kubomoa nyumba na kuharibu miundombinu huku maporomoko ya ardhi yakilazimisha huduma za treni kusitishwa.


Idara ya kudhibiti majanga katika jimbo la KwaZulu-Natal, imewataka watu kukaa nyumbani na kuamuru wale wanaoishi katika maeneo ya mabondeni kuhamia maeneo ya juu.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu