Mabalozi wa Sweden na Finland wazua hasira kwa kuunga mkono wapenzi wa jinsia moja ZambiaBalozi za Sweden na Finland nchini Zambia zinakabiliwa na mzozo nchini humo baada ya kuinua bendera ya upinde wa mvua pamoja na bendera zao za kitaifa kwenye majengo yao siku ya Jumanne.


Mahusiano ya watu wa jinsia moja yameharamishwa nchini Zambia, ambapo sheria za wakati wa ukoloni wa Uingereza kuhusu mapenzi ya jinsia moja bado zinatumika.


Ubalozi wa Sweden nchini Zambia ulituma kwenye ukurasa wake wa Twitter bendera ya upinde wa mvua kwa kutumia alama ya #Idahot2022, ambayo inawakilisha Siku ya Kimataifa ya Kupambana unyanyapaa wa wapenzi wa jinsia moja.


"Haki za LGBTIQ ni haki za binadamu - siku zote na kila mahali," waliandika kupitia twitter.


Ubalozi wa Finland pia aliandika"kusimama pamoja kwa ajili ya haki za binadamu".


Mwanadiplomasia wa zamani wa Zambia Emmanuel Mwamba amedai majibu kutoka kwa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo, tovuti ya The Lusaka Times inaripoti.


"Inashangaza kwamba balozi hizi zilichagua kupeperusha bendera hizi katika majengo yao bila kuzingatia sheria na hisia za kitamaduni za Wazambia na Zambia kuhusu suala hilo," alinukuliwa akisema.


Mnamo Desemba 2019, Amerika ilimwita balozi wake nchini Zambia juu ya mzozo wa kidiplomasia baada ya kukosoa kufungwa kwa wanandoa wa jinsia moja.


Serikali ya Zambia ilikuwa imemshutumu balozi huyo kwa kujaribu kuamuru.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu