Mabaki ya Lumumba likiwemo jino vyarejeshwa DRC,binti yake atoa hotuba ya hisia kaliKatika hafla ya heshima katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, mabaki ya pekee ya kiongozi wa uhuru wa Congo Patrice Lumumba yamerejeshwa kwa familia yake.


Jino lenye taji la dhahabu la kiongozi aliyenyongwa lilichukuliwa na polisi wa Ubelgiji ambaye alikuwa ameshtakiwa kwa kutupa mwili wa waziri mkuu wa kwanza wa Congo.Binti wa Lumumba, Juliana, alitoa hotuba iliyojaa hisia katika sherehe hiyo:


‘’Baba, ndugu zangu na mimi, pamoja na watoto wetu, na vitukuu zako, tumejaribu kupitia hotuba hii, kutafuta maneno ya kukuaga miaka 61 baada ya kutoweka kwako, lakini tunapaswa kukiri kwamba hakuna kinachoweza kueleza kile tunachohisi leo.''


''Tunaweza tu kutamani kwamba popote ulipo, unaweza kujivunia watoto wako, wajukuu zako na vitukuu zako.''


Baba karibu tena nchini, asante. ‘’Tunatamani tu kwamba popote ulipo, ujivunie watoto wako, wajukuu zako na vitukuu zako. Baba karibu tena nchini, asante.’’

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu