Maandamano makubwa yazuka Sudan,ni ya kupinga utawala wa kijeshiMamia ya waandamanaji wanaopinga utawala wa kijeshi nchini Sudan wameandamana jana mjini Khartoum kwa siku ya nne mfululizo.


Mmoja wa waandamanaji hao ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa, wataendelea na maandamano hadi jeshi litakaporudisha utawala wa kiraia kikamilifu.


Maandamano yaliyogeuka na kuwa machafuko Alhamis yalipelekea vofo vya watu 9. Hii ndiyo ilikuwa siku mbaya zaidi ya maandamano kuwahi kushuhudiwa nchini humo kwa miezi kadhaa.


Maandamano ya hivi karibuni yameshuhudia waandamanaji wakichoma magurudumuna kuweka vizuizi barabarani huku maafisa wa usalama wakitumia risasi za moto kuwatawanya waandamanaji.


Tangu mapinduzi ya mwaka uliopita idadi ya waliofariki kutokana na makabiliano na maafisa wa usalama katika maandamano imefikia watu 114.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu