Kundi la Islamic laanza kujisuka upya lamteua kiongozi mkuu mpyaKundi la wanajihad la Islamic state (IS) limeripotiwa kumteua na kumuapisha kiongozi mkuu wao mpya baada ya yule aliekuwa akiliongoza kufariki kwa kujipiga risasi.


Kundi hilo limekula kiapo cha utii kwa kiongozi mkuu huyo mpya Abu Hassan al-Hashemi al-Qurachi, msemaji wa kundi hilo amesema katika sauti iliyorekodiwa, wakati akithibitisha kifo cha kiongozi wa zamani wa IS na msemaji wake wa zamani.


Kifo cha kiongozi huyo wa zamani wa IS pamoja na msemaji wake wa awali pia vimethibitishwa katika sauti iliyorekodiwa.

"Abu Ibrahim al-Hashimi al-Qurachi na msemaji rasmi wa Dola ya Kiislamu, Abu Hamza al-Qurachi waliuawa hivi karibuni,"


Kiongozi wa zamani wa IS alijilipua wakati wa operesheni ya kikosi maalum cha Marekani kaskazini magharibi mwa Syria, eneo lililo chini ya udhibiti wa wanajihadi, Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza Februari 3. mwisho.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu