Kundi la IS laua watu 6 kwa kuwakata vichwa Msumbiji,rais asema aeleza haya



Watu wasiopungua sita wameuwawa kwa kukatwa vichwa na wanamgambo wenye mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS, katika jimbo la Nampula nchini Msumbiji .


Taarifa hizo zimetolewa na rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ambaye amesema mnamo Septemba 6, wanamgambo wenye silaha walifanya mashambulizi katika wilaya za Erati na Memba, wakawakata vichwa watu 6, kuwateka nyara watatu na kisha kuzichoma moto nyumba kadhaa.


Kwa mujibu wa rais Nyusi katika shambulizi hilo wanamgambo sita walikamatwa.



Katika kisa kingine mtawa wa kanisa katoliki raia wa Italia aliuwawa kwa kupigwa risasi usiku wa Jumanne wiki hii wakati kundi lingine la wanamgambo lilipovamia mji wa Nacala.


Rais Nyusi amesema wanamgambo wa itakadi kali wanaoendesha uasi nchini Msumbiji tangu mwaka 2017, wanafanya matukio ya ukatili wakiwa njiani kukimbia operesheni za jeshi la nchi hiyo linalosaidiwa na vikosi vya Rwanda na vile kutoka mataifa ya SADC.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu