Korea Kaskazini yatangaza Lock down kwa mara ya kwanza


Korea Kaskazini imetangaza amri ya kutotoka nje kwa nchi nzima baada ya kudhibitisha maambukizo yake ya kwanza rasmi ya Covid-19.


Vyombo vya habari vya serikali vimeripoti mlipuko wa Omicron katika mji mkuu Pyongyang lakini havikueleza idadi ya visa na maambukizi.


KCNA ilisema ni "tukio kubwa zaidi la dharura" na kwamba kiongozi Kim Jong-un alikuwa katika mazungumzo ya dharura kuandaa namna ya kukabiliana na mlipuko huo kitaifa.


Lakini wachunguzi wanaamini virusi hivyo vimekuwepo nchini kwa muda mrefu.


Korea Kaskazini haijawachanja chanjo ya Covid-19 wananchi wake wala mpango wa chanjo, baada ya kukataa ofa za chanjo ya Sinovac iliyotengenezwa China na AstraZeneca.


Taifa lilikuwa na lengo la kuzuia virusi kwa kufunga mipaka yake tangu kuanza kwa janga hilo, na kusababisha hali mbaya ya kiuchumi na uhaba wa chakula kwani mtiririko wa bidhaa muhimu kwa nchi hiyo masikini ulipungua kwa kiasi kikubwa.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu