Korea kaskazin yaishutumu Korea kusin kuingiza nchini mwao virusi vya Covid 19 kwa makusudiSerikali ya Korea kaskazini imesema mlipuko wa Covid 19 ulianza nchini humo kwa raia wake kugusa "vitu vigeni" vilivyoanguka karibu na mpaka wake wa Korea Kusini.


Wananchi walihimizwa kuwa waangalifu kuzunguka vitu ambavyo vinaweza kuwa vimerushwa katika mpaka kutoka Korea Kusini.

Kwa miaka mingi wanaharakati wa Korea kusini wamerusha maputo kuvuka mpaka kutuma vipeperushi na misaada ya kibinadamu.


Serikali ya Korea kusini katika kujibu shutma hizo imesema "hakuna uwezekano" Covid kuvuka mpaka kwa njia hiyo.


Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini, uchunguzi rasmi uligundua watu wawili ambao waliambukizwa virusi vya Covid 19 mapema katika mlipuko huo baada ya kugusa vitu visivyojulikana karibu na mpaka wa Korea Kusini.


Mwanajeshi mwenye umri wa miaka 18 na mtoto wa miaka 5 walipimwa na kukutwa na virusi hivyo mapema Aprili baada ya kuvipata vitu hivyo kwenye kilima huko Ipho-ri, iliripoti.


Tangu wakati huo, vyombo vya habari vya serikali vilisema: "Virusi vibaya vya Covid-19 vimeenea kwa kasi katika nchini humo"


Serikali ya Korea kaskazini imewaambia wananchi wake kuwa yeyote atakayegundua kitu kisicho cha kawaida aripoti mara moja ili kiweze kuondolewa haraka na timu ya dharura ya kupambana na janga la corona.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu