Kiongozi wa zamani wa Angola Dos Santos amelazwa hospitaliniRais wa zamani wa Angola, José Eduardo dos Santos, amelazwa katika hospitali moja katika mji wa Barcelona nchini Uhispania, shirika la habari la serikali ya Ureno Lusa limeripoti.


"[Bw Dos Santos], amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Barcelona, ​​ambako amekuwa akiishi kwa miaka michache iliyopita," Lusa alisema.


Ripoti hiyo inakuja huku kukiwa na uvumi kuhusu afya ya kiongozi huyo wa zamani wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.


Mnamo Mei, rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 79 alijibu uvumi kuhusu kifo chake kwa kukashifu "ripoti zinazopingana" kuhusu afya yake na kusema kwamba daktari wake wa kibinafsi ndiye pekee aliyeidhinishwa kuzungumza juu ya suala hilo.


Alihudumu kama rais wa Angola kuanzia 1979 hadi 2017.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu