Kenyatta amkataa Ruto licha ya ushindi,Ruto naye amjibu kwa haya hapaRais mteule wa Kenya William Ruto amesema rais anayeondoka madarakani Uhuru Kenyatta hajaona umuhimu wa kumpongeza kwa ushindi wake katika uchaguzi uliompa ushindi dhidi ya Odinga.


‘’Nimeshinda uchaguzi, hilo ndilo la muhimu,bahati mbaya Rais Kenyatta hajaona inafaa kunipongeza lakini nadhani ni sawa, labda amekatishwa tamaa, au hafurahii kwamba nilimshinda mgombea wake. Lakini hivyo ndivyo siasa ilivyo,” aliiambia CNN.


Mahojiano hayo yamerushwa saa chache baada ya Rais Ruto kuweka mtandaoni kuhusu mazungumzo yake ya simu na Rais Kenyatta, ambapo walijadili kuhusu uchaguzi mkuu na shughuli ya mpito kwa utawala mpya.


Ruto, ambaye ni Mkristo muinjilisti, pia aliliambia shirika hilo la habari la CNN kwamba haki za wapenzi wa jinsia moja ‘’si suala kubwa’’ nchini humo kwa sasa, na ataangazia masuala muhimu zaidi ya ukosefu wa ajira na njaa.


‘’Hatutaki kukuza kitu kisicho na umuhimu kukifanya kionekane kuwa na umuhimu mkubwa,hili si suala muhimu kwa watu wa Kenya.’’


Aliongeza: ‘’Suala la mapenzi ya jinsia moja na haki zao litakapokuja, watu wa Kenya watafanya uchaguzi na tutaheshimu chaguo zao,kwa sasa tuangazie masuala yanayoathiri watu wetu.’’


Sheria za Kenya zinaharamisha mapenzi ya jinsia moja nchini humo ambapo adhabu ya kifungo cha hadi miaka 14 jela.


Haijabainika iwapo kumewahi kuwa na hatia ya kufanya mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu