Kenya yamkamata anayesakwa na Marekani kwa biashara ya dawa za kulevyaPolisi wa Kenya wamemkamata mshukiwa anayehusishwa na genge la kimataifa la ulanguzi wa dawa za kulevya na wanyamapori na ambaye alikuwa amefunguliwa mashtaka katika mahakama ya Marekani akiwa na wenzake watatu.


Polisi nchini Kenya ilisema wapelelezi wa Kitengo cha Uhalifu siku ya Jumanne walimkamata Abdi Hussein Ahmed, almaarufu Abu Khadi katika kaunti ya Meru kufuatia taarifa kutoka kwa umma.


Bw Ahmed alishtakiwa mwaka wa 2019 katika mahakama ya Wilaya ya Kusini mwa New York kwa kula njama ya kusafirisha pembe za faru na aina ya tembo wenye thamani ya $7m (£5.7m) na nia ya kusafirisha kilo moja ya kokeini.


Alishtakiwa kwa pamoja na Moazu Kromah almaarufu Ayoub, Amara Cherif almaarufu Bamba Issiaka, na Mansur Mohamed Surur almaarufu Mansour.


Inasemekana walikuwa wamepanga njama ya kusafirisha pembe hizo kutoka Kenya, Uganda, DR Congo, Guinea, Msumbiji, Senegal na Tanzania.


Kukamatwa huko kumewadia baada ya afisa wa Ubalozi wa Marekani Eric Kneedler na mkurugenzi mkuu wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), George Kinoti, kutoa ombi la umma tarehe 26 Mei ili kupata taarifa zinazoweza kusababisha kukamatwa kwa Bw Ahmed.


Mshirika wa Bw Ahmed, Badru Abdul Aziz Saleh, alikamatwa wiki moja baada ya ombi hilo.


DCI ilisema kukamatwa kwa Bw Ahmed na Bw Saleh kuliashiria ‘’ushirikiano wa muda mrefu ambao kurugenzi imekuwa nao na Marekani katika kupambana na uhalifu uliopangwa baina ya mataifa mbalimbali duniani’’.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu