Kenya yakumbwa na kashfa ya ufisadi kuadimika kwa mipira ya KondomuMamlaka ya Ugavi wa Dawa nchini Kenya (Kemsa) inaangaziwa tena, baada ya maelfu ya mipira ya kondomu, vyandarua na dawa za kifua kikuu zenye thamani ya $100,000 (£77,000) kutoweka kwenye ghala lake.


Dawa zilizopotea zinaaminika kuibiwa na kuuzwa tena kimagendo na kwa wanakemia wa kibinafsi, kulingana na Global Fund.

Mfuko huo pia unaituhumu Kemsa kwa kuzidisha thamani ya dawa kwa mamilioni ya dola, huku baadhi ya dawa zikiwa zimeongezwa bei mara 100 zaidi ya bei yake halisi.


Shirika hilo la serikali bado halijazungumzia madai hayo.

Mfuko wa Kimataifa unafadhili mapambano ya Kenya dhidi ya VVU/UKIMWI, kifua kikuu na malaria.

Kemsa iligonga vichwa vya habari mnamo 2020 baada ya ufichuzi wa kashfa ya udanganyifu kukumba ununuzi wa vifaa tiba vya Covid-19.


Zabuni ya thamani ya dola milioni 78 zilisemekana kupewa watu walio na ushawishi wa kisiasa na wafanyabiashara.

Tukio hilo lilimfanya Rais Uhuru Kenyatta kuvunja bodi yake na usimamizi wake mkuu.


Global Fund, ambayo imetoa zaidi ya $1.4m kwa Kenya katika miongo miwili iliyopita, imependekeza uchunguzi zaidi wa Kemsa kuhusu dawa zilizopotea.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu