Kenya kufunga shule kabla ya uchaguziWizara ya Elimu nchini Kenya imeagiza kufungwa kwa shule za msingi za umma kuanzia kesho Jumanne hadi Jumatano tarehe 10 mwezi huu na masomo yatenedlea Alhamisi tarehe 11 .


Taarifa ya wizara hiyo iliyotiwa Saini na Waziri wa Elimu George Magoha imesema uamuzi huu umechukuliwa baada ya mashauriano ili kuruhusu maandalizi ya uchaguzi mkuu unaofanyika Jumanne tarehe 9


Iwapo uchaguzi wa marudio utafanyika endapo mshindi hatopatikana katika duru ya kwanza, tarehe hizo za kufunguliwa kwa shule huenda zinaweza kubadilika na hii inaweza kuathiri mitihani ya kitaifa iliyopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Shule kawaida hutumiwa kama vituo vya kupigia na kujumlisha kila mwaka wa uchaguzi.


Taasisi nyingi ni shule za msingi, sekondari, vyuo vikuu na taasisi za mafunzo ya kiufundi.


Kwa kawaida, uchaguzi wa mwaka huu ungefanyika wakati wanafunzi hawapo shuleni kwa likizo ndefu ya Agosti lakini ratiba hiyo ilivurugwa na janga la Corona lililosababisha shule kufungwa kwa muda mrefu.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu