Kamanda Muliro aibukia Ubungo kulikofanyika uporajiKamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Muliro Jumanne leo amefika kwenye eneo la Msewe Golani Wilaya ya Ubungo ambako usiku wa kuamkia leo mida ya saa tisa Vijana walivamia kwenye nyumba kadhaa ikiwemo hosteli za Mama Msangi na kuibia Watu simu, laptop, pesa za kawaida za matumizi na kuvunja vioo vya magari.


"Tumebaini Wahalifu hawa pia walikua wakisema wanalipiza kisasi cha mwenzao kuuawa, sasa tunachunguza mwenzao aliouawa ni nani na alikua anafanya shughuli gani ? kwahiyo pamoja na tukio hili tunachunguza kwa kina kujua ni kitu gani kilichosababisha tukio hili lifanyike, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam litafatilia na kushughulika nao vikali kama Wahalifu wengine"


“Kila kilichoibwa katika eneo hili kitapatikana, wito wangu mwingine nimeubaini katika eneo hili la Golani mifumo ya kiusalama ya eneo hili imezorota, ni eneo lenye Vijana wengi nguvu kazi ya kutosha lakini mifumo ikiwemo falsafa ya ulinzi shirikishi eneo hili wameiua, hilo nalo ni jambo ambalo nitafatilia”

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu