Jesho Togo lajilaumu kuua vijana liliowafananisha na magaidi,hawakuwa na hatiaJeshi nchini Togo limeelezea kujuta kwa kuwauwa vijana saba wadogo siku ya Jumamosi usiku ambao liliwauwa kimakosa kwa kudhani kuwa walikuwa ni wapiganaji wa jihadi.


Katika taarifa, mkuu wa majeshi wa nchi hiyo, Dadja Maganawe, alisema kuwa kikundi hicho cha vijana kiliuliwa wakati waliposhambuliwa na ndege ua kijeshi wakat iwa ulinzi wa doria wa usiku.


Wahanga wote walikuwa na umri wa kati ya miaka 14 na 18.


Vyombo vya habari katika jimbo la kusini la Savanes viliripoti kuwa vijana hao walikuwa njiani kuelekea nyumbani baada ya kuhudhuria sherehe ya Kiislamu yaEid al-Adha.


Jeshi la Togo limekuw akatika tahadhari ya juu kufuatia shambulio la mauaji la wanamgambo wa jihadi la mwezi Mei, wakati wanajeshi wanane walipouawa karibu na mpaka wa nchi hiyo na Burkina Faso.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu