Iran yanyonga watu 280 ndani ya mwaka mmoja pekee
Iran iliwanyonga watu wasiopungua 280 mwaka jana, kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa jana na mwandishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Iran.


Akiwasilisha ripoti kwa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa, Javaid Rehman amesema idadi ya watu walionyongwa kwa mashtaka yanayohusiana na sheria za mihadarati imeongezeka. Kulingana na ripoti hiyo idadi ya wanawake pia wanaonyongwa imepanda.


Amesema kuna kesi nyingi za unyanyasaji na vitisho dhidi ya familia za wahanga na wengine wanafunguliwa mashitaka ya jinai kwa sababu tu ya kutaka haki itendeke.


Ripoti hiyo inaonyesha kwamba kati ya Januari na Desemba mosi mwaka jana takribani wafungwa 11 wa Kikurdi walikufa gerezani katika hali ambazo hazikuwa wazi.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu