Hungary yaikataa Ukraine yasema haiwezi kuweka vikwazo kwa UrusiWaziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban ametupilia mbali wito wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky wa kutaka silaha na vikwazo vikali dhidi ya Urusi, akisema itakuwa "kinyume na maslahi ya Hungary".


Orban alikataa matakwa ya Zelensky katika Baraza la Ulaya "kwa sababu ni kinyume na maslahi ya Hungary," msemaji wa serikali ya Hungary Zoltan Kovacs alisema katika taarifa.


"Hungary inataka kujiepusha na vita hivi, kwa hivyo haitaruhusu uhamishaji wa silaha kwa Ukraine," Kovacs alisema.

Orban anasema kwamba watu wachache wa kabila la Hungaria magharibi mwa Ukraine wangetishiwa ikiwa Hungary itapeleka silaha Kyiv.


Hungary, mwanachama wa Umoja wa Ulaya na Nato, imekataa kutuma msaada wa kijeshi kwa Kyiv, au kuiruhusu kuvuka mipaka yake. Hata hivyo, imeruhusu zaidi ya wakimbizi nusu milioni wa Ukraine kuingia katika eneo lake.


Orban, mzalendo, amekuza uhusiano wa karibu na Rais wa Urusi Vladimir Putin katika miaka ya hivi karibuni.


Zelensky alitumia hotuba kwa viongozi wa EU siku ya Alhamisi kumtaka Orban kuidhinisha upanuzi wa vikwazo, kuruhusu silaha hadi Ukraine, na kukata uhusiano wa kibiashara na Urusi.


"Sikiliza, Viktor, unajua nini kinaendelea huko Mariupol?" Zelensky alisema, akimaanisha mji wa bandari wa kusini-mashariki wa Ukraine uliozingirwa. "unapaswa kuamua wewe ni nani," alisema.

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu