Hatimaye Mrema anafunga tena ndoa leo


Mrema na mkewe mtarajiwa


Maandalizi kwa ajili ya harusi ya Mwenyekiti wa chama cha Tanzania Labor Part (TLP), Agustino Mrema tayari yamekamilika na tayari wamewasili katika kanisa katoliki parokia ya Uwomboni Kiraracha mkoani Kilimanjaro.


Mrema ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, kuwa mbunge na kugombea urasi wa Tanzania, leo Alhamisi Machi 24, 2022 anafunga tena ndoa baada ya mke wake kufariki mwaka jana.


Mrema alikuwa wa kwanza kutoka nyumbani kwake na kuingia kwenye gari na baadae akatoka bibi harusi akiwa amejifunika kanga hadi usoni ili asionekane na watu.


Picha mbalimbali zinazoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii zinamuonesha mke mtarajiwa akitoka ndani akiwa amefunikwa sura kwa sura kwa kitenge ikiwa ni katika kile kinachoelezwa kuwa ni taratibu za mila za kabila lake.


Hivi karibuni kulizuka gumzo katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii juu ya uamuzi wake wa kuoa tena wengi wakijadili juu ya umri wake .

Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu