Guardiola alalamikia wachambuzi na Media kuibeba Liver poolMeneja wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amevilalamikia vyombo vya habari na wachambuzi kwa kuipendelea Liver pool katika uchambuzi wao na kuiminya klabu yake .


Meneja huyo raia wa Uhispania amesema kila mtu katika taifa la Uingereza anaipendelea Liver pool na wamekuwa wakiipa nafasi kubwa ya kutwaa mataji pale kunapokuwa na ushindani baina ya timu yake na Liver pool.


Katika mahojiano na Bein Sport Guardiola amesikika akisema "Kila mtu katika nchi hii anaunga mkono Liverpool, vyombo vya habari na kila mtu,bila shaka kwa sababu Liverpool ina historia katika mashindano ya Ulaya, Sio kwenye Ligi ya Premia, kwa sababu wameshinda moja katika miaka 30, lakini sio tatizo hata kidogo". Amesema Guardiola
“Hali ndivyo ilivyo, tunatakiwa kupata pointi tisa labda sita, inategemea na mechi mbili zinazofuata kwa tofauti ya mabao" ameongeza


"Sasa Jumatano ndio fainali ya kweli kwetu, hatima yetu iko mikononi mwetu na hii ni muhimu, ndio ukweli " ameeleza.


City watatupa karata yao dhidi ya Wolves Jumatano kabla ya kumenyana na West Ham siku ya Jumapili.


Klabu ya Manchester City itawakosa wachezaji wake Ruben Dias, John Stones na Kyle Walker kwa mechi tatu za mwisho za msimu wa ligi kuu ya nchini Uingereza.


City wako pointi tatu mbele ya Liverpool baada ya kuwalaza Newcastle 5-0 siku ya Jumapili; Guardiola:


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu