Face book na Instagram kuwaruhusu wanaotaka Putin auaweKampuni ya Meta inaomiliki Facebook pamoja na Instagram imeonesha nia ya kutofuta machapisho wala kufungia akaunti za wale wanaotoa wito wa kuuawa kwa rais wa Urusi Vladmir Putin kutokana na uvamizi wa majeshi yake nchin Ukraine.


Katika taarifa ya shirika la habari la Reuters msemaji wa kampuni hiyo ya Meta amesema wanaangalia uwezekano wa kubadilisha sera yake a kutoruhusu machapisho yoyote a uchochezi au kuharibu amani ili kuwaruhusu wale walioathiriwa na vita ya Urusi na Ukraine kuonesha maumivu yao katika mitandao hiyo.


Hata hivyo, kampuni hiyo inasema haitaruhusu wito wa vurugu dhidi ya raia wa Urusi bali itaruhusu wito wa mauaji ya rais Putin na mshirika wake wa Belarus na majeshi yaliovamia Ukraine.


Shirika la habari la Reuters limesema kuwa limeona barua pepe za ndani zinazoelezea mabadiliko hayo ya sera.


"Kwa kuzingatia uvamizi unaoendelea wa Ukraine tuliweka ubaguzi wa muda kwa wale walioathiriwa na vita, kuelezea hisia kali dhidi ya vikosi vinavyovamia," msemaji wa Meta amesema.


Chini ya sera hiyo iliyofanyiwa marekebisho, watumiaji katika nchi zikiwemo Urusi, Ukraine na Poland pia wataweza kutoa wito wa kuuawa kwa Rais Putin wa Russia na Rais wa Belarus Lukashenko.


Barua pepe hizo zinaripotiwa kusema wito wa vifo vya viongozi hao utaruhusiwa isipokuwa kama zitakuwa na malengo mengine, au kujumuisha eneo au mbinu.


Tufuate kupitia:
  • YouTube Social  Icon
  • Twitter Social Icon
  • Black Instagram Icon
  • Facebook Social Icon

Jiunge nasi :

Usipitwe na kitu